IQNA

Mashindano ya Qur'an Kuwait yaanza

11:41 - January 02, 2011
Habari ID: 2056956
Duru ya 15 ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur'an nchini Kuwait imeanza.
Kwa mujibu wa Manal Al Saqri Mkuu wa Mfuko wa Wakfu wa Sayansi za Qur'ani, mashindano haya yanayojumuisha Qiraa na Tajwidi yanafanyika kwa himaya ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu nchini Kuwait.
Ameongeza kuwa duru ya kumi na nne ya mashindano hayo iliwavutia Mahafidh na Maqari wengi wa Qur'ani nchini Kuwait. 'Kuandaliwa tukio hili muhimu la Qur'ani ni jambo litakalopelekea kuibuka kizazi kipya cha Mahafidh wa Qur'ani nchini Kuwait', amesema Al Saqri.
Ameendelea kusema kuwa taarifa kamili kuhusu mashindano ya kitaifa ya Qur'ani zinapatikana katika tovuti ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait yenye anwani ya www.awqaf.org.
722191

captcha