Kwa mujibu wa gazeti la Al Madina, washiriki kutoka nchi 11 wamejiandikisha kushiriki katika kozi hiyo katika siku ya kwanza ya kuzinduliwa.
Riyadh al Muhaidib mkuu wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'ani katika mkoa wa Al Habil amesema kuwa, 'washiriki 20 wa kike kutoka Marekani, Ulaya na nchi za Kiarabu wamejisajili kushiriki katika kozi hiyo. Washiriki wote wanatakiwa kufahamu lugha ya Kiarabu'.
Amesisitiza kuwa kurekebisha fikra potofu za misimamo mikali kunawezekana tuu kwa kupitia uenezwaji mafundisho ya Qur'ani kupitia teknolojia ya kisasa kwa kuzingatia mazingira yaliyopo.
Hivi sasa kuna wanafunzi 8,510 wa kike na kiume ambao wanasoma katika Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'ani katika mkoa wa Al Habil. Jumuiya hiyo inajitahidi kutoa mafunzo ya kuhifadhi Qur'ani na ufahamu wa misingi ya kitabu hicho kitakatifu.
721956