IQNA

OIC yalaani hujuma dhidi ya Kanisa Misri

11:34 - January 02, 2011
Habari ID: 2056958
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu amelaani vikali hujuma ya kigaidi ambayo imelenga raia waliokuwa wakifanya ibada katika kanisa moja huko Alexandria nchini Misri ambapo karibu watu 21 wameuawa na wengine kujeruhiwa Januari Mosi.
Kwa mujibu wa tovuti ya OIC, Ihsanoglu ametuma rambirambi kwa jamaa za waliouawa katika hujuma hiyo na amewaombea waliojeruhiwa kupona haraka. Katibu Mkuu wa OIC ameelezea masikitiko yake makubwa kuwa hujuma hiyo ya kigaidi imesadifiana na sherehe za mwaka mpya.
Ametoa wito kwa watu wa mji wa Alexandria na Wamisri wote kutojiingiza katika njama za kuzusha fitina na kueneza hitilafu miongoni mwa wananchi. Aidha amewataka Wamisri kudumisha umoja na maslahi ya nchi yao mambo ambayo yanawezekana tu kwa kuungana dhidi ya ugaidi ambao hautafautishi baina ya rangi, dhehebu au dini.
722427
captcha