IQNA

Mashindano ya Qur'ani yanalenga kustawisha Uislamu halisi

13:04 - January 03, 2011
Habari ID: 2057510
Kati ya malengo muhimu ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu ni kustawisha mafundisho halisi ya ‘Uislamu wa Mtume Muhammad SAW’ ambao ni kinyume cha Uislamu unaoenezwa na Marekani.
Haya ni kwa mujibu wa Sayyid Ali Sarabi Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Qur'an Iran ambaye ameongeza kuwa, kuarifisha fikra za hayati mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini MA na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei pamoja na misingi ya Qur'ani ya Mapinduzi ya Kiislamu ni mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanachuo Waislamu.
Amesisitiza kuwa kiwango cha mashindano yaliyopita ya Qur'ani kilikuwa kizuri lakini akasema kuna haja ya juhudi zaidi kufanyika kwa ajili ya kuimarisha ufahamu wa mafundisho ya Qur'ani miongoni mwa washiriki wa mashindano hayo.
Amesema Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yatakuwa bora kwa mtazamo wa mipango kuliko yale ya huko nyuma.
Sayyid Ali Sarabi ambaye pia ni mkuu wa Kituo cha Uchapishaji Qur'ani Tukufu nchini Iran amepongeza hatua ya kuongeza kitengo cha wanawake katika mashindano hayo na kusema wanachuo wanawake pia wana uwezo wa kushindana katika viwango cha ufahamu na tafsiri ya Qur'ani.
Amesema mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yatakuwa na baraka nyingi za kimaanawi mbali na kuvunja propaganda chafu dhidi ya Uislamu katika kipindi hiki ambapo kuna wimbi la chuki dhidi ya Uislamu duniani.
Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yatafanyika Januari 9-11 katika mji wa Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran. 716959
captcha