Ahmad al Tayyib Sheikh wa al Azhar ambaye alikuwa akijibu swali kwamba je, kuongozeka kwa idadi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia ni tishio kwa eneo hili? amesema tishio halisi linatokana na uingiliaji wa wageni katika Mashariki ya Kati na ushahidi wa wazi wa jambo hilo ni matukio ya sasa nchini Iraq.
Ameongeza kuwa Marekani iliivamia na kuikalia kwa mabavu Iraq kisha ikaiacha hivihivi na sasa baadhi ya wananchi wa nchi hiyo wanapigana kwa sababu ya masuala ya kimadhehebu, kidini na kimakundi, suala ambalo halikuwepo hapo awali. Sheikh wa al Azhar amesisitiza kuwa mambo haya hayana maslahi kwa Shia wala Suni.
Kuhusu hali ya kisiasa nchini Misri, Sheikh wa al Azhar amesema kuwa hatakati ya Ikhwanul Muslimin inaendesha shughuli za kisiasa nchini humo na al Azhar ni taasisi ya kielimu na kwamba yeye binafsi hapendelei masuala ya kisiasa wala halazimiki kuunga mkono mrengo wowote.
723140