Hayo ni kwa mujibu wa Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ufilipino Bw. Hussein Divsalar. Ameyasema hayo wakati alipokutana na Bw. Nasser Abinal, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Imamiyya na Bassir Datu, mkurugenzi wa jumuiya hiyo.
Divsalar pia amejadili ushirikiano wa Iran katika ujenzi wa maktaba katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia.
Amesema kuwa juhudi za huko nyuma za Idara ya Utamaduni ya Iran huko Ufilipino katika kuanzisha Darul Qur'an katika Msikiti wa Miharlika zilipongezwa na maafisa wa nchi hiyo pamoja na Tume ya Waislamu nchini Ufilipino.
723141