Kikao hicho ambacho kimandaliwa na Muungano wa Vijana wa Kiislamu wa Ufaransa UJM kitawashirikisha wanazuoni, wanafikra na raia wa Kiislamu wa Ufaransa katika Kituo cha Kiislamu cha Tauhidi katika mji uliotajwa.
Tayeb Chouiref, mtarjumi wa vitabu vya kidini na mwandishi wa kitabu cha 'Mafundisho ya Kimaanawi ya Mtume Muhammad (saw)' atahudhuria kikao hicho na kutoa maelezo kuhusu kitabu hicho.
Ni vyema kuasharia hapa kuwa Muungano wa Vijana wa Kiislamu wa Ufaransa unapanga kuandaa vikao kadhaa katika kipindi cha mwaka huu ili kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusiana na wahyi na kuterenshwa kwa Qur'ani Tukufu na vilevile historia ya Kiislamu. 723363