IQNA

Morocco kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani

16:16 - January 04, 2011
Habari ID: 2058858
Mashindano ya 6 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu Tuzo ya Mfalme Muhammad wa Sita yatafanyika tarehe 4 hadi 7 Februari katika mji wa Casablanca nchini Morocco.
Kituo cha habari cha “Marocjournal” kimeripoti kuwa mashindano hayo yatasimamiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Morocco katika nyanja mbili za hifdhi na tartili ya Qur’ani Tukufu.
Taarifa ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Morocco imesema kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa mnasaba wa kuadhimisha Maulidi ya Mtume Muhammad (saw).
Sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo zitafanyika Ijumaa tarehe 5 Februari katika ukumbi wa mikutano wa shule ya Qur’ani ya Msikiti wa Mfalme Hassan wa Pili katika mji wa Casablanca. 723871
captcha