Katika mkutano na Tuti Alawiya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Shafi’iyah ambaye pia ni mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wanawake Waislamu, Muhammad Ali Rabbani mwambata wa utamaduni wa Iran nchini Indonesia amejadili maandalizi ya harakati kadhaa za utamaduni kwa mnasaba wa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Maafisa hao wawili waliafiki kushirikiana katika kuandaa semina ya kimataifa kuhusu ‘Ulimwengu wa Kiislamu na Majukumu ya Mwanamke Muislamu’ na vilevile kuandaa tamasha ya utamaduni na sanaa itakayohudhuriwa na wanawake kutoka nchi mbili.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa chuo kikuu cha Kiislamu ambapo pande mbili ziliafiki kufungua Taasisi ya Masomo ya Iran na Uislamu na vilevile kuandaa masomo ya lugha ya Kifarsi katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Shafi’iyah .
723947