Katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Nchi Kavu la Iran Januari 3 washindi wakiwemo wa Mashindano ya 9 ya Wanachuo wa Jeshi walitunukiwa zawadi na vyeti vya heshima.
Hafla hiyo ilianza kwa kisomo cha Qur'ani Tukufu na baada ya hapo kamanda wa jeshi la nchi kavu la Iran Brigedia Jenerali Ahmad-Reza Pourdastan alihutubia hadhara hiyo akisema, ‘harakati za Qur'ani katika jeshi la nchi kavu ni za kuvutia’.
Mashindano hayo yalifanyika Desemba 20-23 katika viwango tafatui vya kuhifadhi sehemu au Qur'ani kamili, qiraa na ufahamu wa Qur'ani na vilevile adhana.
Walioshikilia nafasi za kwanza watashiriki katika Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya Vikosi vya Jeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo yanatazamiwa kufanyika mwezi Mei 2011.
723589