IQNA

Semina ya Qur'ani na Familia kufanyika Marekani

11:45 - January 06, 2011
Habari ID: 2059843
Semina ya Qur'ani Tukufu na Familia imepangwa kufanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Marekani ikisimamiwa na Taasisi ya Bayyinah.
Tovuti ya Bayyinah imeripoti kuwa lengo la kuitishwa semina hiyo ni kujibu matakwa ya familia za Kiislamu katika nyanja za masuala ya Qur'ani na kuzihamasisha katika suala la kuimarisha uhusiano wao na Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu.
Katika mfululizo huo huo semina ya "Qur'ani na Familia: Suratul Rahman" imepangwa kufanyika tarehe 8 Januari katika Kituo cha Kiislamu cha mji wa Monroeville katika jimbo la Pennsylvania na "Qur'ani na Familia: Suratu Yasin" tarehe 15 Januari katika Kituo cha Kiislamu cha New England katika mji wa Sharon jimboni Massachusetts.
Semina hizo zitahutubiwa na mwasisi wa kiuo cha Kiislamu cha Bayyinah Norman Ali Khan akichunguza masuala mbalimbali yanaozungumziwa katika sura za Rahman na Yasin. 724293

captcha