IQNA

Bunge la Misri launga mkono pendekezo la al Azhar

11:40 - January 06, 2011
Habari ID: 2059844
Mkuu wa Kamisheni ya Masuala ya Kidini katika Bunge la Misri Mahmoud al Sharif ameunga mkono pendekezo la Jumuiya ya Uhakiki wa Kiislamu ya al Azhar la kushadidisha adhabu kwa wanaochapisha nakala zenye makosa za Qur'ani Tukufu na hadithi za Mtume (saw)..
Mamoud al Sharif amesema Kamisheni ya Masuala ya Kidini ya Bunge la Misri itaunga mkono muswada huo wa al Azhar.
Tarehe 31 Disemba Jumuiya ya Uhakiki wa Kiislamu ya al Azhar ilitoa pendekezo la adhabu ya kifungo cha miaka 15 jela, faini ya lira elfu tano na kusimamishwa kazi miaka mitatu kama adhabu ya taasisi yoyote itakayochapisha Qur'ani na hadithi za Mtume (saw) zenye makosa ya kichapa.
Muswada huo utajadiliwa katika kikao kijacho cha Jumuiya ya Uhakiki wa Kiislamu ya al Azhar kabla ya kuwasilishwa bungeni kwa ajili ya kupasishwa. 724283

captcha