IQNA

Malaysia kufungua maabara ya bidhaa halali

13:10 - January 08, 2011
Habari ID: 2060229
Serikali ya Malaysia imetangaza kuwa itafungua maabara ya kukagua bidhaa halali mwakani.
Hayo yamesemwa na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Jamil Khir Baharom ambaye amesema Malaysia ina matumaini kuwa itakuwa nchi ya kwanza kuwa na maabara kama hiyo ya kukagua bidhaa halali kwani maabara ya sekta binafis ndio yamekuwa yakitumiwa. Amesema maabara hiyo itasimamiwa na Idara ya Ustawi wa Kiislamu ya Malayasia. ‘Maabara hii situ kuwa itafanya utafiti kuhusu bidhaa za vyakula bali pia bidhaa nyinginezo na itatumiwa na wateja wa kitaifa na kimataifa’, amesema Waziri Khir Baharom baada ya kutembelea Maabara ya Taasisi ya Bidhaa Halali ya Malaysia.
Ameongeza kuwa Binge la Malaysia litabuni Sheria ya Bidhaa Halali. Amesisitiza kuwa baada ya sheria hiyo kuidhinishwa, Idara ya Ustawi wa Kiislamu ya Malayasia ndio taasisi pekee itakayotoa vibali vya bidhaa halali na kwa hivyo sekta binafsi haitakuwa na ruhusa ya kutoa vibali hivyo.
724942
captcha