IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ni motisha kwa wanachuo

13:25 - January 08, 2011
Habari ID: 2060231
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yatawapa motisha wanachuo ili waweza kujibidiisha na hivyo kupata mafanikio zaidi.
Hayo ni kwa mujibu wa Mkuu wa Kituo cha Darul Qur'ani nchini Iran Mehdi Qaresheikhloo alipozungumza na IQNA kuhusu Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu ambayo yanatazamiwa kufanyika Januari 9-11 Januari katika mji wa Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran.
Amesema moja ya matokeo ya mashindano hayo ni kuwahimiza vijana kuimarisha uwezo wao wa sayansi na maarifa ya Qur'ani.
Amekosoa baadhi ya mashindano ya Qur'ani ambayo hayatilii maanani viwango na kusema kuna washiriki wa kimataifa ambao hawateuliwi kwa njia zinazofaa jambo ambalo huenda likatia doa itibari ya mashindano yanayoandaliwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amesema washiriki Wairani hupitia mitihani migumu kabla ya kuteuliwa kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.
Qaresheikhloo ambaye binafsi ni qarii wa Qur'ani amesisitiza kuhusu umuhimu wa mawasiliano baina ya maqarii wa Qur'ani na wataalamu kutoka nchi mbalimbali na kusema mawasiliano kama hayo yatainua viwango vya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.
715834
captcha