Mick Ramsy afisa anayesimamia masuala ya elimu katika Kituo cha Mawasiliano ya Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Waterloo amesema kuwa kibali cha kugawa bure nakala za Qur’ani kati ya wanafunzi na familia zao kimetolewa na Idara ya Elimu ya eneo hilo.
Ameongeza kuwa wawakilishi wa kituo hicho wataanza kugawa bure nakala za kitabu kitukufu cha Qur’ani kwa wanafunzi katika mwaka mpya wa masomo.
Mick Ramsy amongeza kuwa hatua hiyo imechukuliwa kwa lengo la kuarifisha Uislamu na Qur’ani Tukufu kwa wanafunzi wa eneo hilo.
Amesema kwa sasa jumuiya za Kiyahudi na Kikristo zinajishughulisha na kazi ya kugawa bure nakala za Taurati na Injili katika maeneo mbalimbali ya Canada. 725676