Hassan Bayadi ambaye pia ni mwanachama wa baraza la sera katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo amesema Baraza la Mji wa Tehran linajitahidi kupata idhini ya Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC kuanzisha makao makuu ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu nchini Iran.
Amesisitiza kuhusu umuhimu wa mashindano ya Qur'ani ya kimataifa na kusema maandilizi yake ni hatua inayopaswa kupongezwa ambayo imechukuliwa na Jumuiya ya Harakati za Qur'ani ya Wanachuo wa Iran.
Amesema mbali na baraka zake nyingi za kisiasa, kijamii na kimataifa, mashindano hayo yanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kustawisha utamaduni wa dini halisi ya Kiislamu kama ilivyotangazwa na Mtume Muhammad SAW na vilevile kuimarisha umoja wa Kiislamu.
Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanachuo Waislamu yataanza Jumapili tisa Januari katika mji mtakatifu wa Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran ambapo wawakilishi wa nchi 40 wanatazamiwa kushiriki.
718421