Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni (ISESCO) limetoa mchango wa kifedha kwa Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu katika mji wa Mash'had, Iran, ili kuandaa Awamu ya Tatu ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yanayoanza Januri 9-11.
Mashindano hayo yanawashirikisha wanachuo Waislamu kutoka nchi 40 duniani. ISESCO itawakilishwa katika mashindano hayo na Dkt. Abbas Sadri, Mkurugenzi wa Idara ya Kieneo ya ISESCO mjini Tehran.
ISESCO ilianzishwa na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC mwezi Mei mwaka 1979. ISESCO ni kati ya taasisi kubwa zaidi ya Kiislamu zinazoshughulikia masuala ya elimu, sayansi na utamaduni na makao yake makuu yako mjini Rabat, Morocco.
726122