Kwa mujibu wa tovuti ya Journal Online, ujumbe wa Ufilipino uliotumwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York imeifahamisha Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo kwamba pendekezo hilo limepitishwa kwa sauti moja na Baraza Kuu la umoja huo.
Akizungumzia suala hilo, mwakilishi wa kudumu wa Ufilipino katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa kupitishwa azimio hilo ni hatua muhimu katika juhudi za kubuni ulimwengu unaozingatia misingi ya wastani, amani na maendeleo. Amesema jambo hilo pia linaweka wazi thamani za kidini katika kutatua changamoto za kimataifa na kuleta amani duniani.
Sisitizo la ustawi wa utamaduni katika kufikiwa malengo ya milenia ya tatu, umuhimu wa kushirikishwa watu wote katika jamii na hasa wanawake na vijana katika kueneza utamaduni wa mazungumzo kati ya dini na tamaduni, nafasi ya vyombo vya habari katika kueneza utamaduni huo na kuandaliwa kikao cha mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) ili kujadili suala hilo ni mambo yalisisitizwa katika azimio hilo. 727274