Kwa mujibu wa gazeti la Al Dastur, mkutano huo umeandaliwa na tawi la Jordan la Kamati ya Wahandisi wa Quds kwa lengo la kuchunguza hali ya mji mtakatifu wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Kujadili ukiukaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na utawala wa Kizayuni, kutaka ulimwengu wa Kiislamu uchukue hatua kuhusu kadhia ya Quds ambayo ni muhimu sana kwa Waislamu, kuchunguza sera haribifu za utawala wa Kizayuni dhidi ya Quds pamoja na malengo yake haramu ya kuuyahudisha mji huo ni kati ya mada zinakazojadiliwa katika kikao hicho.
Washiriki pia wanajadili njia za kulinda turathi takatifu za kiutamaduni na kiustarabu za Quds na vilevile njia za kueneza utulivu katika maisha ya Wapalestina. 727582