IQNA

Mashindano ya Qur'ani yanatangaza mafundisho ya Kiislamu

14:28 - January 11, 2011
Habari ID: 2062559
Kufanyika mashindano ya Qur'ani ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika kiwango cha kimataifa ni hatua muhimu katika kufikia umoja wa Kiislamu na kueneza mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.
Hayo yamesemwa na Al Harith Ibrahim Al Mikshafi mwakilishi wa Sudan katika kiwango cha hifdhi katika Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo wa Kiislamu alipohojiwa na mwandishi wa IQNA katika ukumbi wa mashindano hayo yanayofanyika katika mji mtakatifu wa Mash'had kaskazini-mashariki mwa Iran. Ameongeza kuwa, 'Wamagharibi ambao wamekuwa wakiukosea heshima Uislamu na kuwatusi Waislamu bila shaka hawafurahishwi na tukio kama hili la mashindano ya Qur'ani'.
Ameongeza kuwa, mahafidh wa Qur'ani walio katika mashindano ya tatu ya Qur'ani ya wanachuo Waislamu wana uwezo mkubwa sana na kwa hivyo mashindano ya sasa ni magumu sana.
Mwanachuo huyo wa Sudan amesema serikali ya Khartoum huandaa mashindano ya Qur'ani kuanzia mashinani hadi taifa.
Al Harith Ibrahim Al Mikshafi ni mwanafunzi wa Kitivo cha Tilawa ya Qur'ani katika Chuo Kikuu cha Qur'ani na Sayansi za Kiislamu mjini Khartoum nchini Sudan na alianza kuhifadhi Qur'ani akiwa na umri wa miaka 7 na sasa ana umri wa miaka 20.
727933
captcha