Kwa mujibu wa gazeti la Arab News la Saudi Arabia, utawala wa Kizayuni una azma ya kubomoa nyumba hiyo uliyoighusubu katika eneo la Sheikh Jarrah na kujenga mahala pake jengo la Kizayuni, jambo linalokwenda kinyume kabisa na sheria za kimataifa.
Katibu mkuuwa OIC amesema kuwa kwa mujibu wa azimio nambari nne la Geneva utawala ghasibu wa Israel hauna haki ya kubomoa nyumba na maeneo ya Quds katika ardhi unazozikalia kwa mabavu kwa lengo la kujenga majengo mapya katika maeneo hayo. Ihsanoglu ameongeza kuwa OIC itaendelea kufanya juhudi za kuzuia hatua hizo haribifu za utawala haramu wa Israel. Amezitaka nchi na taasisi husika za kimataifa kuchukua hatua za lazima kwa ajili ya kusimamisha mara moja vitendo hivyo vya utawala wa Israel vinavyokwenda kinyume kabisa na maazimio pamoja na sheria za kimataifa. 727729