Hayo yamesemwa na Badruddin Abdulhakiim, mwakilishi wa Libya katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yanayomalizika leo katika mji mtakatifu wa Mash'had. Amesema kuwa mashindano hayo yamefanyika kwa kiwango cha juu katika upande wa idadi ya washiriki na ubora wake na ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuandaa vyema mashindano hayo.
Badruddin Abdulhakiim ambaye anashiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano kama hayo ya kimataifa amesema kuwa suhula zilizopo, utaratibu wa mashindano na makazi ya washiriki yametayarishwa kwa njia nzuri mno.
Badruddin Abdulhakiim ambaye ni mwanafunzi wa udaktari katika Chuo Kikuu cha al Fatih mjini Tripoli amewahi kushiriki katika mashindano mengi ya Qur'ani nchini kwake na kupata nafasi mbalimbali. Amesema Kitabu cha Mwenyezi Mungu Qur'ani kina taathira kubwa katika pande mbalimbali za maisha ya mwanadamu na kwamba kusoma Qur'ani Tukufu kunaimarisha hali ya kujiamini na kuna nafasi muhimu katika mafanikio ya kielimu na kijamii. 728088