IQNA

Mkuu wa Baraza la Waislamu Ghana:

Waislamu wajiepushe na mwenendo usio wa Kiislamu

21:15 - January 11, 2011
Habari ID: 2063105
Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini Ghana amewataka Waislamu nchini humo kujiepusha na mienendo isiyo ya Kiislamu na vitendo vinavyosababisha hitilafu na mtengano katika jamii.
Ibrahim Alkad amewataka Waislamu wa Ghana kujiepusha na husuda, kiburi, chuki na mambo mengine yanayokwenda kinyume na maadili mema ya kijamii.
Sheikh Ibhahim Alkad ameliambia shirika la habari la Ghana katika mji wa Kumasi kwamba: "Sisi Waislamu tunalazimika kuwa kigezo bora cha maisha mema kwa watu wa jamii."
Amesema Waislamu na wafuasi wa dini nyingine wanapaswa kumuomba Mwenyezi Mungu ili awasamehe dhambi zao na kuwaangalia kwa jicho la huruma. 728831
captcha