Hati hiyo ilitolewa alasiri ya jana katika ukumbi wa mikutano wa IRIB katika mji mtakatifu wa Mash'had ambako ndiko Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yalikofanyika.
Sehemu ya hati hiyo inasema: "Kijana mwema Rahim Khaki ni miongoni mwa makarii hodari wa Qur'ani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye anayesoma Qur'ani kwa umahiri mkubwa na mwenye vipaji vya aina mbalimbali katika medani hiyo".
Hati hiyo imesema: "Rahim Khaki ni miongoni mwa wahudumu wa Qur'ani Tukufu na mimi Abul Ainain Shuaisha ninamzawadia hati hii karii huyu hodari wa Iran."
Ustadh Abul Ainain Shuaisha amesema mwishoni mwa maandishi ya hati hiyo kwamba: "Ninamuomba Mwenyezi Mungu Muweza ampe taufiki ya kushikamana na sheria za tilawa karii Rahim Khaki na wanafunzi wake."
Sherehe za kufunga duru ya tatu ya Mashindano ya Kimataifa ya Wanachuo Waislamu zilifanyika jana usiku tarehe 11 Januari kwa kutangazwa washindi katika nyanja za hifdhi na kiraa katika mji mtakatifu wa Mash'had huko kaskazini mashariki mwa Iran. 728943