Kamati hiyo itakuwa na jukumu la kupendekeza masharti ya kushiriki katika mashindano, sehemu mashindano yatakapofanyika, matangazo yake na kiasi cha zawadi watakazopewa washindi.
Kamati hiyo aidha inaweza kuwaalika watu kutoka nje wenye uzoefu ili watoe mchango wao katika kuandaa mashindano hayo ya Qur'ani.
Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani ya Qatar kwa kawaida huwa na sehemu saba zinazojumuisha kuhifadhi Qur'ani kamili, kuhifadhi juzuu 25, kuhifadhi juzuu 20, kuhifadhi juzuu 15, kuhifadhi juzuu 10, kuhifadhi juzuu 5 na kuhifadhi juzuu ya mwisho ya Qur'ani Tukufu.
Raia wa Qatar na wageni waishio nchini humo wanaruhusiwa kushiriki katika mashindano ya kuhifadhi Qur'ani kamili na sehemu zilizobakia zitawashirikisha raia wa Qatar pekee.
728702