IQNA

Mahafidh wa Qurani wanapaswa kuwa kigezo katika Jamii

12:51 - January 12, 2011
Habari ID: 2063401
‘Jukumu la mahafidh wa Qur'ani ni muhimu sana katika jamii’, amesema mwakilishi wa Syria katika Mashindano ya Tatu ya Qur'ani ya Kimataifa ya Wanachuo Waislamu.
Yasin Mamdooh Al Hamuee ambaye ni hafidh wa Qur'ani nzima amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa mahafidh wa Qur'ani wanapaswa kuwa na tabia njema na kigezo bora katika jamii na watekeleze mafundisho ya Qur'ani katika maisha yao binafsi.
Amesisitiza kuwa wale wote walio katika harakati za Qur'ani Tukufu wanapaswa kuwa na tabia na akhlaki njema na kuongeza kuwa, ‘Qur'ani inatuongeza katika amali njema’.
‘Qur'ani Tukufu imebadilisha maisha yangu na kunifundisha somo la kutopoteza matumaini katika hali ngumu maishani’ amesisitiza Al Hamuee.
Al Hamuee anasomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Damascus nchini Syria na alianza kuhifadhi Qur'ani akiwa na umri wa miaka 7. Ni mara ya kwanza anashiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanachuo Waislamu ambayo yalimalizika tarehe 11 Januari katika mji mtakatifu wa Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran.
728006
captcha