Kwa mujibu wa tovuti ya BruDirect nuskha hizo zimeandamana na tarjumi za Kiingereza na Kifarsi za aya za Qur'ani.
Haji Jaafari bin Haji Suheili, mkuu wa shule hiyo amepokea nuskha hizo kutoka kwa Muhammad Ashtiyani, Balozi wa Iran nchini Brunei. Balozi Ashtiyani ametangaza kuwa ubalozi huo una mpango wa kusambaza nuskha zaidi za Qur'ani katika shule zote za Brunei.
Amesema tarjumi hizo za Qur'ani zimechunguzwa na kupitishwa na taasisi na vituo mbalimbali vinavyojushughulisha na masuala ya Qur'ani nchini Iran. 729221