IQNA

Washindi wa Mashindano ya Qur'ani ya Wanachuo Iran

12:46 - January 13, 2011
Habari ID: 2063875
Jopo la majaji katika Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu limetangaza kuwa wawakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameshika nafasi za kwanza katika vitengo viwili vya qiraa na hifdhi ya Qur'ani nzima.
Muhammad Khatibu na Hamid Valizadeh walishika nafasi za kwanza katika hifdhi na qiraa.
Katika hifdhi mshindi wa pili alikuwa Badruddin Abdul Hakim al Warfani kutoka Libya na wa tatu alikuwa Muhammad Salim Ghazali kutoka Indonesia.
Mwakilishi wa Afghanistan Sayyid Hamidullah Hashemi na Sayyid Thamaruddin Samadov wa Tajikishtan walishika nafasi ya pili na ya tatu katika qiraa.
Washindi wa kwanza wa mashindano hayo wametunukiwa zawadi ya dola elfu kumi kila mmoja, nafasi ya pili dola elfu nane na nafasi ya tatu dola elfu tano. Washindi hao wote pia wametunukiwa loho na nishani ya mashindano ya sasa ya Qur’ani ya wanachuo wa Kiislamu.
Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yalifanyika Mash'had kuanzia Januari 9-11 na kuwashirikisha maqarii na mahafidh kutoka nchi 40 duniani.
728944
captcha