IQNA

Jumba la Makumbusho ya Qur'an la Iran kupata jengo jipya

12:48 - January 13, 2011
Habari ID: 2063886
Jengo jipya la Jumba la Kitaifa la Makumbusho ya Qur'ani nchini Iran litafunguliwa mezi Februari kwa mnasaba wa siku za Alfajiri Kumi za maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Hayo ni kwa mujibu wa mkuu wa jumba hilo Fakhroddin Saberi ambaye amesema jumba hilo litakuwa katika jengo Arg-e-Azadi katika makutano ya Barabara za Azadi na Yadegar-e-Imam.
“Jengo la sasa liko karibu na ofisi ya rais na kwa mujibu wa sheria za trafiki kuna vizingiti kwa wanaotaka kutembea hapo”.
Kwingineko amesema kuna mipango ya kuandaa maonyesho yenye anwani ya: “Turathi yenye thamani ya Qur'ani na Mapinduzi ya Kiislamu” sambamba na maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
728448
captcha