Vijana sita wa Kishia katika mji wa Ihsaa Saudi Arabia wanaendelea kuzuiliwa katika jela za mji huo kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa bila kuhukumiwa mahakamani, kwa kisingizio cha kuweka mabango ya Ashura katika mji huo.
Vijana hao ambao ni wanachuo na wafanyakazi wa serikali wote wanatoka katika mtaa wa ar-Ramliya katika mji wa Ihsaa.
Katika miaka iliyopita pia walikamatwa na wenzao wengine wa mji wa Ihsaa kwa visingizio tofauti visivyo na msingi.
Wazazi na familia za vijana hao katika kipindi hiki chote wamekuwa wakionana na viongozi wa mji huo ikiwemo Wizara ya Mambo ya Ndani ili kuzungumzia kuachiliwa huru kwa vijana hao lakini bila mafanikio yoyote.
Mashambulio dhidi ya wombolezaji wa Ashura katika mji wa Ihsaa pamoja na kufungwa misikiti na mashule ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mji huo limekuwa jambo la kawaida ambalo hufanywa mara kwa mara na maafisa usalama wa Saudia dhidi ya Washia wa nchi hiyo. Maafisa usalama wa Saudia pia hawawapi Mashia fursa ya kushiriki kwenye minasaba tofauti ya vifo na kuzaliwa viongozi wao wa kidini. 730136