IQNA

Kituo cha Kwanza cha Mashia chafunguliwa Niger

10:43 - January 16, 2011
Habari ID: 2065061
Kituo cha kwanza cha Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Niger kimefunguliwa katika Jimbo la Maradi.
Kituo hicho kilichojengwa kwa kutegemea misaada ya Mashia wa eneo hilo kilifunguliwa Januari 15. Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe za ufunguzi wa kituo hicho zilianza kwa kusomwa Qur'ani Tukufu na baada ya hapo dua maalumu imesomwa kabla ya kuzindua kituo hicho.
Akizungumza katika sherehe hiyo Sheikh Muhammad Sanusi ameashiria umuhimu wa kuanzisha kituo cha Waislamu wa madhehebu ya Shia na kusema kuwa: ‘Kituo hiki kitakuwa na nafasi muhimu katika kuwafahamisha watu kuhusu Uislamu na madhehebu ya Shia. Aidha kituo hiki kitakuwa na darsa maalumu za Qur'ani pamoja na mihadhara ya kidini”.
Naye Abdulkarim Yusumai mmoja kati ya viongozi wa Mashia nchini Niger amesema kuanzishwa kituo cha Mashia katika Jimbo la Maradi kutaongeza mawasiliano baina ya Mashia.
Katika hafla hiyo washiriki wamekusanya kiasi kikubwa cha fedha za kusaidia kujengwa vituo vya Mashia katika maeneo mengine ya Niger.
726436
captcha