IQNA

Bunge la Iran launga mkono harakati za Qur'ani

10:56 - January 16, 2011
Habari ID: 2065087
Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) imetangaza kuwa itaidhinisha mapendekezo ya serikali kuhusiana na masuala ya Qur'ani.
Hayo ni kwa mujibu wa Sayyid Javad Zamani msemaji wa kamati ya bunge ya masuala ya kijamii ambaye alikuwa akizungumza na mwandishi wa IQNA kuhusu sera za utamaduni kama sehemu ya Mpango wa Tano wa Maendeleo nchini Iran.
Zamani amesema kuwa viongozi na wananchi wote wa Iran wamepata mafanikio kutokana na kufuata mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Amesema wabunge wanajitahidi kuhakikisha kuwa maamuzi yao yote katika Majlisi yanafanyika kwa mujibu wa mafundisho ya Qur'ani. Amesema mwaka huu Majlisi itapitisha bajeti maalumu ya harakati za Qur'ani nchini Iran. 730315
captcha