IQNA

Misikiti ya Bosnia yachomwa moto

14:07 - January 16, 2011
Habari ID: 2065366
Kwa mujibu wa tangazo la Waziri wa Mambo ya Ndani wa Bosnia Herzegovina hivi karibuni misikiti kadhaa ilichomwa moto nchini humo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Kuwait KUNA, waziri huyo amesema kuwa hakihusishi chama chochote cha kisiasa na tukio hilo. Taarifa iliyotolewa na waziri huyo inasema kuwa uchunguzi uliofanywa haujaweza kubaini wahusika hasa wa tukio hilo la uchomaji moto misikiti.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bosnia Herzegovin imewataka wananchi wa nchi hiyo kuwa watulivu na kutochukua hatua zozote zinazoweza kuvuruga utulivu na amani ya nchi hiyo hadi uchunguzi utakapokamilika na wahusika kuadhibiwa na vyombo husika.
Msikiti wa kale wa Sarayevo ni miongoni mwa misikiti iliyoshambuliwa katika tukio hilo. 731004
captcha