Hayo yamesemwa na Muhammad Hussein Yadegari Mkuu wa Jumuiya ya Jihadi ya Vyuo Vikuu nchini Iran. Katika mazungumzo na IQNA, Yadegari amesema mashindano kama hayo huandaa mazingira ya kuwahimiza na kuwaongoza wanafunzi wa vyuo vikuu kufahamu zaidi mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Akiashiria Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanachuo Waislamu yaliyofanyika wiki iliyopita mjini Mash'had, amesema kuwa, "hatupaswi kumalizia shughuli zetu katika mashindano ya Qur'ani tu. Kuna haja ya kutoa mafunzo kwa makarii na mahafidh mahiri na kujitahidi kufafanua kuhusu shughuli zetu za Qur'ani".
"Kwa kuanzisha mitandao ya kijamii kwa msingi wa Qur'ani Tukufu, makarii na mahafidh wa Qur'ani kote duniani wanaweza kujuana zaidi na kuchukua hatua za kueneza harakati za Qur'ani katika uga wa kimataifa", ameongeza Dkt. Yadegari.
Ameendelea kusema kuwa mpango wa kuanzisha mitandao ya kijamii kwa msingi wa Qur'ani Tukufu ni katika mipango inayopewa kipaumbele na Jumuiya ya Wanachuo wa Iran ya Harakati za Qur'ani .
730994