IQNA

Utawala haramu kupasisha mpango wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi Quds Tukufu

17:02 - January 17, 2011
Habari ID: 2066284
Utawala haramu wa Israel umeazimia kupasisha mpango wa ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Quds Tukufu licha ya upinzani mkali wa wapenda uhuru kote duniani na nchi za ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya siasa za kidhalimu za utawala huo.
Shirika la habari la Kuwait KUNA limenukuu maandishi ya gazeti la Haaretz la Israel kwamba mradi huo wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi huko Quds unasubiri kupasishwa na Kamisheni ya Mipango ya Quds na kwamba iwapo utapasishwa nyumba 1400 za walowezi zitajengwa katika eneo la Bait Jala Quds Tukufu.
Limeandika kuwa inatazamiwa kuwa mpango huo utakabiliwa na upinzani mkali kutoka pembe mbalimbali duniani.
Utawala wa Kizayuni wa Israel tayari umejenga nyumba elfu 8 katika eneo hilo la Bait Jala Quds Mashariki.
Utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukiharibu na kuvunja turathi za Kiislamu za mji mtakatifu wa Quds kwa miaka mingi sasa huku jumuiya za kimataifa zikinyamaza kimya. 731884


captcha