IQNA

Hafla za Qur'ani katika sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

12:47 - January 18, 2011
Habari ID: 2066419
Kamati ya Qur'ani katika sherehe za Alfajiri 10 imetangaza mipango yake katika maadhimisho ya mwaka wa 32 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Mahdi Gharasheikhlu Mkuu wa Taasisi ya Darul Qur'an inayoshughulikia harakati za Qur'ani katika maadhimisho hayo amesema taasisi za Qur'ani kote nchini Iran zimeandaa programu maalumu katika siku 10 za maadhimisho hayo.
Amezitaja programu hizo kuwa ni pamoja na kuandaa vikao vya Qur'ani katika mikoa mbalimbali, mashindano ya Qur'ani, tamasha za Qur'ani kwa ajili ya watoto, vijana na familia ni kati ya programu zilizopangwa katika idara mbalimbali za kuhubiri Uislamu.
Kati ya hafla hizo ni ile itakayofanyika Februari 4 chini ya anuani ya "Mapinduzi ya Kiislamu, Qur'ani, Itrat na Kumsubiri Mwokozi". Hafla hiyo pia itawaenzi wataalamu wa Qur'ani katika jamii na kuwapa vijana motisha kujifunza sayansi za Qur'ani.
Aidha katika maadhimisho ya mwaka wa 32 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu misahafu 40 elfu itasambazwa katika vituo mbalimbali vya Qur'ani kote nchini Iran na washindi wa mashindano ya Qur'ani ya Nurul Huda III pia watazawadiwa.
729497

captcha