Abbas Salimi ambaye aliongoza jopo la majaji katika mashindano hayo amesema Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo yalikuwa fursa nzuri kwa vijana kuwafahamu wataalamu na wasomi wa Qur'ani Tukufu. Ameongeza kuwa aghalabu ya washiriki katika viwango vya qiraa na hifdhi walikuza vipawa vyao kwa kiwango kikubwa.
Ustadh Salimi amesema wanachama wote katika jopo la majaji walikuwa na uzoefu mkubwa na wanafahamika kimataifa. Amesema vitengo vingine kama vile utafiti kuhusu masuala ya Qur'ani vinaweza kuongezwa katika mashindano yajayo.
730973