Kwa mujibu wa gazeti la Al Dastoor, mradi huo unajumuisha kuihifadhi Qur'ani nzima na itatekelezwa kwa muda wa miaka mitano.
Mradi huo umeandaliwa na Chuo cha Darul Arqam ambacho kinafungamana na Jumuiya ya Kiislamu ya Misaada Jordan.
Msimamizi wa mradi huo ni Muhammad al Majali Mkuu wa Chuo Kikuu cha Utafiti cha Jordan ambaye pia ni mkuu wa Jumuiya ya Kuhifadhi Qur'ani ya Jordan.
"Wanafunzi wataweza kuhifadhi Qur'ani nzima kwa muda wa miaka mitano. Kila mwaka watahifadhi Juzuu Sita", amesema mkurugenzi wa Chuo cha Darul Arqam Bw. Khalis Asghar.
Ameongeza kuwa wanafunzi pia wataelimishwa kuhusu tajweed na sheria za kusoma Qur'ani kwa kuzingatia kanuni za usomaji wake.731877