Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la al-Anbaa, mashindano hayo yanaandaliwa na Idara Kuu ya Vijana na Michezo ya Kuwait kwa ushirikiano wa Idara ya Masuala ya Qur'ani inayofungamana na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu. Mashindano hayo yamepangwa kufanyika katika makundi mawili ya vijana walio na umri wa miaka 10 hadi 16 na 17 hadi 29. Mshindi wa kwanza wa mashindano hayo atapewa zawaidi ya dinari 500 za Kuwait, wa pili dinari 400, wa tatu dinari 300, wa nne dinari 200 na wa tano dinari 150.
Idara Kuu ya Vijana na Michezo ya Kuwait imewataka vijana walio na hamu ya kushiriki kwenye mashindano hayo kusajili majina yao kupitia anwani ifuatayo ya mtandao: www.islam.gov/quran au kufika kwenye ofisi za idara hiyo katika eneo la ar-Raq'i. Muhula wa mwisho wa kusajili majina hayo ni tarehe tarehe 3 Februari.
Idara hiyo imetangaza kuwa lengo la mashindano hayo ni kuandaa mazingira ya mashindano kati ya vijana kuhusiana na masuala ya kidini na kiutamaduni. Imewataka vijana kushiriki kwa wingi katika mashindano hayo ili kunyanyua kiwango chao cha malezi bora ya nafsi. 731847