Shirika rasmi la habari la nchi hiyo Bernama, limesema kuwa licha ya kutumika bajeti hiyo katika shughuli iliyotajwa, pia itatumika katika uendeshaji wa shughuli za misikiti kupitia mtandao wa intaneti.
Waziri wa Sayansi na Teknolojia wa Malaysia ambaye alikuwa akizungumza katika sherehe ya kuhitimu wanafunzi wa masomo ya Qur'ani huko katika mkoa wa Sarawak amesema kuwa kufikia sasa hatua nyingi zimechukluliwa kwa lengo la kutengwa bajeti hiyo na kwamba inatazamiwa kuongezwa katika siku zijazo kwa ajili ya kuimarisha shughuli za Qur'ani nchini humo. 732115