Televisheni na redio za Tunisia zimeanza tena kurusha hewani adhana za swala mbalimbali baada ya kuzuiwa kwa miaka mingi katika utawala wa dikteta aliyeng'olewa madarakani wa nchi na kukimbilia Saudi Arabia Zainul Abidin bin Ali. Redio na televisheni za taifa za Tunisia Jumapili iliyopita zilikata matangazo ya kawaida na kutangaza adhana baada ya kupigwa marufuku kwa miaka mingi katika utawala wa kidikteta uliong'olewa madarakani.
Kanali ya saba ya televisheni ya Tunisia ilikata matangazo yake ya kawaida na kuanza kutangaza adhana kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 50 na baadaye kidogo idadi kubwa ya vijana wa Tunisia ilimiminika mitaani na kusimamishwa swala ya jamaa.
Serikali ya Tunisia katika kipindi cha utawala wa Habib Bourguiba na dikteta wa nchi hiyo Zainul Abidin bin Ali aliyeongoza Tunisia kwa ngumi ya chuma kwa kipindi cha miaka 23 ilipiga marufuku adhana katika vyombo rasmi vya dola na hata kuzuia swala za ijumaa katika nchi hiyo ambayo karibu wananchi wake wote ni Waislamu. Dikteta Bin Ali pia alikuwa akizuia swala za jamaa misikitini na alipiga marufuku ibada na ada nyingi za Kiislamu likiwemo vazi la heshima la mwanamke wa Kiislamu hijabu. 732608