IQNA

Mashindano ya hifdhi ni makali zaidi kuliko qiraa

13:31 - January 19, 2011
Habari ID: 2067061
Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yalishuhudia mchuano mkali zaidi katika hifdhi kuliko qiraa.
Haya ni kwa mujibu wa Amir Aghai ambaye alikuwa katika jopo la majaji wa mashindano hayo yaliyofanyika Januari 9-11 katika mji wa Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran.
“Ikilinganishwa na mashindano yaliyopita, tumeona ishara za kustawi kiwango cha mashindano”, amesema na kuongeza kuwa hilo limeshuhudiwa zaidi katika kitengo cha hifdhi.
Ametoa wito kwa wanaoandaa mashindano hayo kuzingatia zaidi uwezo wa washiriki wa kigeni kutokana na kuwa baadhi walikuwa dhaifu. Ustadh Amir Aghai ambaye amehifadhi Qur'ani nzima amesema kitengo cha qiraa hakijastawi sawia na hifdhi na kuongeza kuwa kuna haja ya juhudi kufanyika kuimarisa qiraa.
Mbali na washiriki kutoka mwenyeji wa mashindano yaani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, washiriki kutoka nchi kama vile Libya, Morocco , Algeria, Syria, Iraq na Tunisia walionyesha ustadi mkubwa na ndio sababu ushindani mkubwa unakuwa miongoni mwa washiriki kutoka nchi hizo, amesema Ustadh Aghai.
731087
captcha