IQNA

Warsha ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu yafanyika

13:38 - January 19, 2011
Habari ID: 2067063
Warsha ya Tano ya “Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu na Mshikamano wa Umma wa Kiislamu” imefanyika katika Chuo Kikuu cha Madhehebu za Kiislamu mjini Tehran.
Kwa mujibu wa Sayyed Mahdi Tabataba’i mhadhiri katika Kitengo cha Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu katika chuo hicho amesema warsha hiyo itajadili mafanikio ya kuleta umoja wa Kiislamu nchini Kuwait.
Sheikh Hussein Ma’tuq mwanazuoni mashuhuri wa Kuwait amewasilisha makala katika warsha hiyo iliyofanyika Januari 19 katika Ukumbi wa Imam Musa Sadr chuoni hapo.
Kubainisha fikra ya kukurubisha madhehebu ya Kiislamu na umoja wa Kiislamu pamoja na mbinu zinazotumika kufikia malengo hayo na matatizo yaliyopo ni kati ya mada zilizojadiliwa katika kikao hicho.
732852
captcha