IQNA

Tovuti ya Suna za Mtume SAW yaanzishwa

13:34 - January 19, 2011
Habari ID: 2067064
Tovuti ya kwanza kuhusu Suna za Mtume SAW imezinduliwa nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mkurugenzi wa tovuti hiyo Muhammad Adnan amesema pia kuna sehemu ya lugha ya Kiingereza ambayo ina maelezo kuhusu maisha ya Mtume SAW.
Kati ya yaliyomo katika tovuti hiyo ni masuala ya ibada, dua, sala na familia, ubinadamu, ustaarabu, miuzija ya Qur'ani na maadili mema kwa mtazamo wa Suna za Mtume Muhammad SAW.
Adnan ameongeza kuwa kuarifisha Suna za Mtume Muhammad SAW kupitia haki za binadamu, elimu, uhusiano wa kimataifa, elimu ya familia na umoja wa kijamii ni kati ya malengo mengine ya tovuti hiyo.
Ameelezea matumaini kuwa tovuti hiyo itaarifisha sura halisi ya Suna za Mtume SAW kupitia kutangaza maadili bora ya Kiislamu.
Tovuti hiyo imezinduliwa na Idara ya Kutangaza Uislamu mjini Riyadh.
732290
captcha