Tovuti ya Muslimness imeripoti kuwa kanali hiyo ya televisheni itakuwa na vipindi vya Kiislamu kwa makundi ya rika tofauti na mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Televisheni hiyo itakuwa ikitoa huduma kwa Waislamu milioni 20 wa Russia ambao ni moja ya saba ya jamii nzima ya nchi hiyo.
Mufti Mkuu wa Russia Rawil Gaynetdin amesema anaamini kuwa kueneza moyo za kuvumiliana kati ya wafuasi wa dini mbalimbali ni jambo lenye udharura mkubwa.
Waislamu wa Russia wanatarajia kwamba kufunguliwa kanali hiyo ya televisheni kutapunguza ubaguzi wanaokabiliana nao katika nchi yao wenyewe. Vilevile wanasisitiza kuwa televisheni hiyo ya Kiislamu itadhihirisha sura halisi ya Uislamu na Waislamu wa Russia. 733508