IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya watoto yamalizika Gambia

19:31 - January 19, 2011
Habari ID: 2067653
Mashindano ya Qur'ani makhsusi kwa ajili ya watoto wenye umri wa kati ya miaka 7 na 18 yalimalizika Jumanne tarehe 18 Januari katika mji wa Karawan nchini Gambia.
Mashindano hayo ambayo yamesimamiwa na Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu ya Karawan yalimalizika kwa kuomba msaada kwa Baraza la Waislamu wa Gambia kuzisaidia kifedha shule za Qur'ani nchini humo.
Mashindano hayo ambayo yamefanyika kwa shabaha ya kustawisha zaidi elimu ya Kiislamu, kutoa mafunzo ya Qur'ani kwa kizazi cha vijana na kuzidisha ushirikiano kati ya jumuiya na taasisi za Kiislamu nchini Gambia, yamewashirikisha wanafunzi wa shule za miji mbalimbali ya nchi hiyo.
Mwishoni mwa mashindano hayo washindi walitunukiwa zawadi. 733549
captcha