Far'han as-Shaidi, mkuu wa kamati ya kielimu ya kongamano hilo amesema kuwa kikiwa ni kituo muhimu cha utamaduni wa mazungumzo ya kidini na uenezwaji wa misimamo ya kuvumiliana na kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini tofauti, mji mtakatifu wa Najaf una nafasi muhimu katika kubuni mbinu na sera za masomo katika uwanja huo.
Amelaani kulengwa makundi ya waumini wa dini nyinginezo zisizo za Kiislamu na kutaka zichukuliwe hatua za dharura kwa madhumuni ya kupambana na uovu huo. Amewataka maimamu na mahatibu wa misikiti mbalimbali kutumia nafasi zao kuhubiri ujumbe wa wafuasi wa dini tofauti kuishi pamoja kwa amani na kujiepusha kutumia mimbari zao katika kuhubiri chuki na ugaidi dhidi ya watu wengine.
Akizungumza katika kongamano hilo, Kheiri Buzani, mkuu wa kamati ya wafuasi wa dini za wachache katika eneo la Kurdestan la Iraq amewataka wafuasi wa dini zote za mbunguni kuishi pamoja kwa amani na kusikitishwa na hali ya kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitumia vibaya taasisi za kidini kwa madhumuni ya kufikia malengo yao binafsi.
Wawakilishi wa dini tofauti za kidini walishiriki katika kongamano hilo.733468