Tovuti ya Islam Today imeripoti kuwa Naibu Meya wa mji wa Strasbourg anayeshughulikia masuala ya dini amesema kuwa misikiti hiyo itajengwa kwa shabaha ya kutatua matatizo ya Waislamu ambao wanalazimika kutekeleza swala mabarabarani na katika maeneo mengine kutokana na kutowepo misikiti. Amesema hatua hiyo imechukuliwa licha ya makundi yenye misimamo mikali kudai kwamba ujenzi wa misikiti nchini Ufaransa ni tishio kwa utambulisho wa nchi hiyo.
Moja ya misikiti hiyo miwili ambao utakuwa na uwezo wa kupokea watu 600 hadi 800 utajengwa katika eneo lenye ukubwa wa hekta 10 kwa gharama ya uro milioni 2.2. Msikiti mwingine wa pili ambao ni mdogo utagharimu yuro laki 8 na 47 elfu katika eneo lenye ukubwa wa hekta 4.5.
Halmashauri ya mji wa Strasbourg itatoa msaada wa yuro laki tatu kwa ajili ya ujenzi wa misikiti hiyo. 733437