IQNA

Hati ya Kishia Duniani Kuchapishwa

13:04 - January 20, 2011
Habari ID: 2067843
Hujjatul Islam Ali Ansari Buyer Ahmadi, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kishia amesema utayarishaji Hati ya Kishia Duniani uko katika ajenda kuu ya taasisi hiyo.
Akizungmza na mwandishi wa IQNA, amesema kuwa, "Wataalamu 100 wa Uislamu hivi sasa wanafanya utafiti kuhusu hati hiyo".
Akisisitiza kuhusu udharura wa kuchapisha hati hiyo, amesema kuwa sababu ya wafuasi wa dini zinginezo kuwa na shaka kuhusu Uislamu ni kwa sababu ya kutojua misingi ya Uislamu. "Tunakusudia kuarifisha taswira ya kweli ya Uislamu duniani", ameongeza.
Hujjatul Islam Ali Ansari Buyer Ahmadi amesema kuna Mashia milioni 400 kote duniani na kuongeza kuwa, Mashia duniani wanapaswa kueneza ujuzi wao kuhusu Uislamu.
732372
captcha