IQNA

Profesa Mjerumani asilimu

11:07 - January 22, 2011
Habari ID: 2068172
Profesa katika Chuo Kikuu cha Hamburg Ujerumani amesilimu baada ya kusoma kwa kina mafunzo ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Noor, Profesa Harald Schneider amesilimu na kuamua kufuata madhehebu ya Shia wakati akifanya utafiti katika mji wa Karbala nchini Iraq.
Profesa Harald Schneider ametoa taarifa akisema: “Nilikuwa nimesafiri kwa mara ya pili katika mji mtakatifu wa Karbala. Mara hii nilipoingia katika Haram Takatifuya Imam Hussein , nilipata hisia nzuri ambayo siwezi kuifafanua kwa maneno, hisia ambayo nilikuwa sijawahi kuipata maishani”.
Harald Schneider amechagua jina la Kiislamu la Hassan na kuongeza kuwa, “itikadi za madhehebu ya Shia daima zinaenda sambamba na fikra zangu binafsi”.
Abdul Mahdi Karbalai, msimamizi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS amemfahamisha profesa huyo Mjerumani historia fupi ya matukio ya kusikitisha ya Karbala na vilevile malengo ya harakati ya Imam Hussein AS.
733515
captcha